Yeroboamu I

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yeroboamu I
Remove ads

Yeroboamu I (kwa Kiebrania ירבעם השני au יָרָבְעָם; kwa Kigiriki Ιεροβοάμ; kwa Kilatini Jeroboam) alikuwa mwana wa Nebati akatawala kwa miaka 22 Ufalme wa Israeli baada ya makabila 10 ya kaskazini kuasi ukoo wa Daudi wakati wa mjukuu wake Rehoboamu.

Thumb
Yeroboamu akihalalisha sanamu mbili za Ndama ya dhahabu; mchoro katika Bible Historiale, 1372).

Biblia inamhukumu hasa kwa kuanzisha sera ya kidini iliyowataka Waisraeli wamuabudu YHWH kwa sura ya fahali ya dhahabu katika mahekalu ya Dani na Beteli ili wasiende Yerusalemu, mji mkuu wa ufalme wa ukoo wa Daudi

Remove ads

Historia

William F. Albright alikadiria ufalme wake kudumu tangu mwaka 922 KK hadi 901 KK, wakati E. R. Thiele alisema kuwa alitawala tangu 931 KK hadi 910 KK.[1]

Katika Biblia

Agano la Kale linamtaja mara nyingi kama chanzo cha dhambi kuu ya Waisraeli ambayo hatimaye ilisababisha ufalme uangamizwe na Waashuru katika karne ya 8 KK.

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads