Yosefu Barsaba

From Wikipedia, the free encyclopedia

Yosefu Barsaba
Remove ads

Yosefu Barsaba (pia Yusto, yaani "Mwadilifu") alikuwa mmojawapo kati ya wafuasi wa kwanza wa Yesu.

Thumb
Wanafunzi 70 wa Yesu, akiwemo Yosefu Barsaba.

Kwa msingi huo, baada ya kifo cha Yuda Iskarioti, akawa mmoja kati ya wawili waliopendekezwa kushika nafasi yake kama mtume, lakini bahati ilimuangukia Mathia (Mdo 1:21-26).

Hata hivyo alifanya bidii katika uinjilishaji[1]. Mapokeo ya Kikristo yanasimulia kwamba baadaye akawa askofu wa Eleutheropoli, alipofia dini.

Anaheshimiwa hivyo na Wakatoliki, Waorthodoksi na Waarmenia kama mfiadini kwa jina la mtakatifu Yusto wa Eleutheropoli. Aliweza kuwa mmojawapo kati ya wakazi wengi waliouawa na Vespasian mwaka 68[2].

Sikukuu yake huadhimishwa nao tarehe 20 Julai[3], 30 Oktoba na 9 Aprili.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads