Yosefu Maria Robles
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yosefu Maria Robles (kwa Kihispania José Maria Robles Hurtado, Mascota, Jalisco, Mexico, 3 Mei 1888 - Quila, Jalisco, 26 Juni 1927) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki nchini Meksiko hadi alipouawa kwa kutundikwa mtini bila kesi wakati wa Vita vya Wakristero.

Kwa miaka 14 alikuwa amehudumia kwa upendo mkubwa waamini wake, pamoja na kuandika vitabu vya Kikristo na kuanzisha shirika la Masista wa Moyo Mtakatifu wa Yesu[1].
Papa Yohane Paulo II alimtangaza mwenye heri tarehe 22 Novemba 1992 halafu mtakatifu mfiadini tarehe 21 Mei 2000 pamoja na wenzake 24 waliofia dini katika vita hivyo[2]:
Sikukuu yao inaadhimishwa kila tarehe 21 Mei ila ya kwake mwenyewe ni tarehe ya kifodini chake[3].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads
