Yosefu wa Studion
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Yosefu wa Studion (Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 760 hivi – Thessalia, Ugiriki, 15 Julai 832) alikuwa mmonaki kama familia yake yote, pia mtunzi wa tenzi na matini mengine ya liturujia[1], halafu askofu mkuu wa Thesalonike kuanzia mwaka 806/807 hadi alipoondolewa madarakani.
Anakumbukwa pia kwa kumlaumu kaisari na kwa kutetea kwa nguvu picha takatifu, bila kujali kwamba msimamo wake ulimvutia tena na tena dhuluma pamoja na kaka yake Theodoro wa Studion hata akafariki uhamishoni kwa njaa[2].
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu mfiadini.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads