Theodoro wa Studion
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Theodoro wa Studion (Konstantinopoli, leo nchini Uturuki, 759[1] – Cape Akritas, Bitinia, 826) alikuwa mmonaki, halafu abati wa monasteri ya Studion mjini.[2]

Aliifanya kuwa shule ya wasomi, watakatifu na wafiadini wahanga wa dhuluma za waliopinga heshima kwa picha takatifu. Kwa kutetea kwa nguvu heshima hiyo, bila kujali kwamba msimamo wake ulimvutia dhuluma kutoka kwa kaisari na patriarki zilizoathiri sana afya yake, alipelekwa uhamishoni mara tatu [3].
Pia alishika nafasi muhimu katika kufufua umonaki na fasihi huko Bizanti.
Akiheshimu sana mapokeo ya Mababu wa Kanisa na ili kufafanua imani sahihi aliandika vitabu maarufu kuhusu mada za msingi wa mafundisho ya Kikristo.
Kati ya vitabu vyake vingi, barua kuhusu urekebisho wa monasteri ndiyo maandishi ya kwanza kupinga utumwa.[4][5]
Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 11 Novemba[6] au 12 Novemba.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads