Ziara ya Bikira Maria

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ziara ya Bikira Maria
Remove ads

Ziara ya Bikira Maria (pia: Maamkio) ni ile iliyofanywa na Mama wa Yesu, alipokuwa mjamzito tangu siku chache, kwa Elizabeti, aliyekuwa na mimba ya miezi sita katika uzee wake (Lk 1:39–56[1][2]). Lengo lilikuwa kumhudumia hadi ajifungue mtoto, Yohane Mbatizaji, miezi mitatu baadaye[3][4].

Thumb
Mchoro wa ukutani wa Kiorthodoksi katika kanisa la Mt. George huko Kurbinovo, Masedonia Kaskazini.

Kadiri ya Injili, walipokutana tu, Roho Mtakatifu alimjaza kwanza Yohane Mbatizaji awe nabii, tena zaidi ya nabii (Math 11:9), naye aliruka kwa shangwe tumboni mwa mama yake, tena Elizabeti mwenyewe aliyetambua ujauzito wa Maria na hivyo kumpongeza kuwa mbarikiwa kuliko wanawake wote na mwenye heri kwa kuwa alisadiki kwamba aliyoambiwa na Bwana yatatimia.

Akiitikia unabii wao, Maria alimtolea Mwenyezi Mungu utenzi wa sifa maarufu kwa jina la neno lake la kwanza katika Kilatini, Magnificat [5].

Tukio hilo la kusisimua linaadhimishwa na madhehebu mbalimbali ya Ukristo tarehe 31 Mei[6][7] au 2 Julai[8] katika Ukristo wa Magharibi na 30 Machi [9] au Jumapili mojawapo ya Majilio [10] katika Ukristo wa Mashariki.

Katika Rozari linakumbukwa kama fumbo la pili la furaha[11].

Pia limekuwa asili ya kazi nyingi za huruma na sanaa ya Kikristo.

Remove ads

Habari katika Injili

Siku zile Mariamu aliondoka, akaenda upesi eneo la milimani katika mji wa Yuda; Aliingia katika nyumba ya Zakaria na kumsalimia Elizabeti. Ikawa, mara Elizabeti aliposikia salamu ya Mariamu, mtoto tumboni mwake akaruka kwa furaha; na Elizabeti akajazwa Roho Mtakatifu; na akasema kwa sauti kuu, akasema: «Umebarikiwa wewe katika wanawake na mzao wa tumbo lako amebarikiwa; na anijilie wapi mama wa Bwana wangu? Kwa maana, mara sauti ya salamu yako ilipofika masikioni mwangu, mtoto tumboni mwangu aliruka kwa furaha. Mwenye furaha yule ambaye ameamini kwamba yale aliyoambiwa kutoka kwa Bwana yatatimizwa!” (Injili ya Luka 1:39-45)

Remove ads

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads