Ziwa Assal

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ziwa Assalmap
Remove ads

Kwa ziwa lenye jina la karibu angalia Assale (Ethiopia)

Ukweli wa haraka Mahali, Anwani ya kijiografia ...

Ziwa Assal (kwa Kifaransa Lac Assal) ni ziwa la chumvi lililopo nchini Jibuti. Liko katika mpaka wa kusini wa mkoa mwa Tadjoura, ikigusa eneo la mkoa wa Dikhil, takribani km 120 magharibi mwa Mji wa Jibuti.

Liko m 155 chini ya usawa wa bahari katika Bonde la Afar. Fuo zake zinashirikisha eneo la chini zaidi barani Afrika na ni ya pili ya chini zaidi duniani baada ya Bahari ya Chumvi huko Israeli/Palestina/Jordan.

Urefu wake mkubwa unafikia kilomita 19 na upana wake mkubwa hadi km 7; eneo la maji yake ni hadi km² 54. Kina cha juu kinafikia hadi mita 40. Beseni lake inajumlisha maeneo ya km² 900.

Ziwa hili halina njia ya kutoka kwa maji isipokuwa uvukizaji. Tokeo lake, ilhali maji ya kuingia yana kiasi cha chumvi ndani yake, ni kwamba kiwango cha chumvi katika maji ya ziwa kinazidi kuongezeka. Leo hii ni ziwa lenye chumvi nyingi duniani [1] kushinda Bahari ya Chumvi.

Eneo la ziwa hili ni kama jangwa na hakuna mimea wala wanyama waonekanao ila mimea midogo katikati ya ziwa hilo.

Kipimo cha juu cha halijoto katika eneo hilo hufanya maji kugeuka ukungu kwa urahisi, kwa hiyo eneo hilo limezungukwa na mwamba wa chumvi iliyoshikamana.

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads