Jibuti (mji)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Jibuti (kwa Kiarabu جيبوتي) ni mji mkuu na mji mkubwa nchini Jibuti ukiwa na wakazi 400,000.


Mji wenyewe uko kwenye rasi inayogawa Ghuba ya Aden kutoka Ghuba ya Tadjoura, 11°36' kaskazini, 43°10' mashariki (11.60, 43.1667).
Remove ads
Historia
Mji huo ulianzishwa na Ufaransa kama bandari mwaka wa 1888, ukawa mji mkuu mwaka wa 1891, ukiandamwa na Tadjourah.
Msafiri mmoja mwandishi alielezea mji Jibuti kama mji ulio na shida ya kujitambulisha, alisema ya kwamba "mji wa kudumu kwa taifa la wahamiaji, ni mji wa Kiafrika uliotengenezwa kama makao ya Kiulaya na pia kama Hong Kong wa Kifaransa kwa Bahari ya Shamu."
Mji pamoja na bandari ulianzishwa kwa sababu mahali pake pana umuhimu wa kijeshi kwa kuwa uko karibu na mlango wa bahari wa Bab el Mandeb ulio njia ya kuingia Bahari ya Shamu kutoka Bahari Hindi na kuelekea mfereji wa Suez.
Wakati wa ukoloni ulikuwa muhimu kwa Ufaransa kwa sababu meli zake ziliweza kupumzika hapa na kuongeza maji na makaa njiani kati ya Mediteranea na makoloni ya Kifaransa huko Vietnam na kandokando yake.
Remove ads
Hali ya sasa
Mji umepangwa na Wafaransa na sehemu mbili: moja kwa ajili ya maafisa Wafaransa na nyingine kama makazi kwa ajili ya Waafrika.
Kaskazini mashariki kuna bandari inayotumika kwa biashara za kimataifa, uvuvi wa samaki na feri inayoenda Obock na Tadjoura.
Hulka za mji wa Jibuti ni mapwa kwa pwani ya magharibi na soko kubwa la kati, na uwanja wa michezo wa taifa, Jumba la Rais na Msikiti Hamouli.
Gari la moshi laenda hadi Addis Ababa, na pia mji huu, wasafiri wa ndege hushukia Uwanja wa Ndege wa Jibuti-Ambouli
Remove ads
Tazama pia
Viungo vya nje
- Satellite picture by Google Maps (ramani na picha za makala ya Google)
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jibuti (mji) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads