Zuonosia
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Zuonosia (kutoka Kiingereza: zoonosis, zoonotic desease) ni ugonjwa wa kuambukiza wenye asili ya mnyama unaosababisha ugonjwa wa binadamu.
Magonjwa ya zuonosia huenea kwa njia ya bakteria, virusi, fungi au vimelea[1].
Magonjwa hayo hutokea mara nyingi. Imekadidiriwa kuwa mnamo asilimia 60 za magonjwa ya kuambukiza yote ni ya zuonosia, yaani maambukizo hupitia wanyama au wadudu.[2]
Njia za maambukizi
Maambukizi hutokea kiasili hasa kwa njia mbili
- mnyama mgonjwa anapitisha kiambukizi moja kwa moja hadi binadamu (mfano: kichaa cha mbwa kinapitishwa pale ambako virusi vyake vinaingia mwilini mwa binadamu, kwa kawaida mtu aking'atwa na mbwa mgonjwa).
- kupitia vekta (vector):
- kiambukizi kutoka mnyama mgonjwa kinahamia mnyama mwingine asiyegonjeka lakini anapitisha kiambukizi kwa binadamu (mfano: bakteria za tauni huambukiza panya; kutoka kwa panya mgonjwa huingia pia katika viroboto wanavyonyonya damu yao. Viroboto hao hawana tatizo na bakteria lakini wananyonya pia damu ya binadamu. Kwenye hatua hiyo kiambukizi kinapitishwa kwa binadamu na kusababisha tauni kwake.
- viambukizi vingine huishi ndani ya mnyama bila kusababisha ugonjwa kwake. Vimelea aina ya plasmodium vinavyosababisha malaria huishi ndani ya mbu za jenasi anopheles. Wakati wa kumdunga mtu mbu anapitisha kwa binadamu vimelea hivyo ambavyo vinasababisha homa ya malaria.
Remove ads
Magonjwa mbalimbali ya zuonosia
Magonjwa yanayosababishwa na chakula
Magonjwa mengi yanayotokana na chakula ni magonjwa ya zuonosia. Hapo mwanadamu anagonjeka kutokana na kula kitu ambacho kilitoka kwa mnyama mgonjwa.
Viambukizi vya kawaida ambavyo husababisha magonjwa kupitia chakula ni bakteria wa salmonella, campylobacter, na escherichia coli (E. coli). Mayai, samaki, nyama ya kuku, na maziwa vinaweza kubeba bakteria hao na kusababisha magonjwa yanayotokana na chakula, kama usumisho wa chakula, kwa wanadamu. [3] [4]
Magonjwa ya zuonosia yanayoambukizwa kupitia chakula ni pamoja na:
Mara nyingi, watu wanaweza kuzuia maabukizi kupitia chakula kwa kukipika kwa muda wa kutosha na hivyo kuua bakteria au vimelea vilivyomo. [5]
Maambukizi ya moja kwa moja
Yafuatayo ni mifano ya magonjwa ya zuonosia ambayo wanadamu wanaweza kuambukizwa moja kwa moja kutoka kwa wanyama wagonjwa walio hai.
Magonjwa ya zuonosia yanayoambuiza kupitia vekta
Remove ads
Magonjwa mapya kutokana na virusi badilifu
Kuna virusi mbalimbali ambavyo kwa kawaida vinapatikana kwa wanyama vinavyoweza kubadili tabia kadhaa na kupata uwezo wa kuathiri binadamu.
Mabadiliko ya aina hiyo yametazamwa hasa kwa virusi vya influenza[11] vya ndege, nguruwe na farasi, halafu kwa virusi vya corona[12].
Wakati virusi vya wanyama vinapata uwezo wa kusambaa kutoka mtu hadi mtu, vinaweza kuathiri watu wengi kwa sababu ni "virusi vipya". Maana mwili hupambana na virusi kwa uwezo wa mfumo wa kingamaradhi (immune system) unaochungulia virusi na kutoa zindikomwili (antibodi) zenye uwezo wa kuzuia virusi. Mfumo wa kingamaradhi hukumbuka mashambulio ya miaka ya nyuma, lakini virusi vipya ni changamoto kwa mfumo huo. Kama virusi vipya kutoka mnyama fulani ni tofauti sana na vyote vilivyotangulia uwezo wake wa kusababisha hatari kali ya afya ni mkubwa. Hapa kuna uwezekano wa mlipuko wa maambukizi (epidemia, hata pandemia) jinsi ilivyotokea kwenye tauni ya karne za kati, na influenza ya 1918.
Marejeo
Tovuti za Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads