Fira , swila au kobra (Unguja ) ni nyoka wenye sumu ambao ni wana wa nusufamilia Elapinae katika familia Elapidae . Kwa lugha za Ulaya huitwa “cobra” ambalo ni kifupi cha cobra de capelo , jina la Kireno lamaanishalo “nyoka mwenye ukaya”. Wanaposumbuliwa nyoka hawa hujiinua na kupanua shingo zao kama ishara ya hatari. Spishi kadhaa hutema sumu kwa nguvu na hulenga macho. Sumu hii ikiingia kwa macho isababisha upofu wa muda.
Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Fira
Fira shingo-nyeusi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya:
Animalia (Wanyama)
Faila:
Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila:
Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli:
Reptilia (Wanyama wenye damu baridi na magamba ngozini)
Oda:
Squamata (Mijusi, mijusi-nyungunyungu na nyoka)
Nusuoda:
Serpentes (Nyoka)
Familia:
Elapidae (Nyoka walio na mnasaba na fira )
Nusufamilia:
Elapinae
Ngazi za chini
Jenasi 6:
Funga
Aspidelaps lubricus , Swila Pua-kigao Kusi (Cape coral snake )
Aspidelaps scutatus, Swila Pua-kigao Mabaka (Shield-nosed cobra )
Hemachatus haemachatus , Fira Koo-baka (Rinkhals )
Naja anchietae , Swila wa Anchieta (Anchieta's cobra )
Naja annulata , Swila-maji Milia (Banded water cobra )
Naja annulifera , Swila Milia (Snouted cobra )
Naja ashei , Fira Mkubwa (Ashe's spitting cobra )
Naja christyi , Swila-maji wa Kongo (Congo water cobra )
Naja haje , Swila Mkubwa au Swila wa Misri (Egyptian cobra )
Naja katiensis , Swila wa Mali (Mali cobra )
Naja melanoleuca , Swila-misitu (Forest cobra )
Naja mossambica , Fira wa Msumbiji (Mozambique spitting cobra )
Naja multifasciata , Swila Mchimbaji (Burrowing cobra ) - Inaainishwa katika Paranaja pia
Naja nigricincta , Fira Milia (Zebra spitting cobra )
Naja nigricollis , Fira Shingo-nyeusi (Black-necked spitting cobra )
Naja nivea , Swila Kusi (Cape cobra )
Naja nubiae , Fira Nubi (Nubian spitting cobra )
Naja pallida , Fira Mwekundu (Red spitting cobra )
Naja senegalensis , Swila Magharibi (Senegalese cobra )
Pseudohaje goldii , Swila-miti wa Gold au Mgoli (Gold's tree cobra )
Pseudohaje nigra , Swila-miti Mweusi (Black tree cobra )
Walterinnesia aegyptia , Swila-jangwa (Desert cobra )
Ukweli wa haraka
Simple English Wiktionary
Wikamusi ya Kiswahili ina maelezo na tafsiri ya maana ya neno:
Funga
Swila pua-kigao kusi
Fira koo-baka
Swila-maji milia
Swila milia
Swila mkubwa
Swila wa Mali
Swila-misitu
Fira wa Msumbiji
Fira milia
Swila kusi
Fira mwekundu
Swila-jangwa