Nyoka

reptilia wanaotamba na wana damu baridi From Wikipedia, the free encyclopedia

Nyoka
Remove ads

Nyoka ni watambaachi au reptilia wasio na miguu. Kuna takriban spishi 3,000 duniani: wako kwenye mabara yote nje ya Antaktiki na Aktiki.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Kama reptilia wote wana damu baridi na ngozi ya magamba. Wote ni wala nyama na spishi mbalimbali hutumia sumu kwa kuvionda lakini nyoka walio wengi hawana sumu wanashika windo kwa miili yao au kwa mdomo tu.

Wote wanazaa kwa njia ya mayai lakini spishi kadhaa hubeba mayai ndani ya mwili hadi wadogo wamekua tayari.

Mijusi wasio na miguu wanafanana sana na nyoka lakini nyoka hawana makope machoni wala masikio ya nje.

Kuna nyoka wadogo wenye sentimita kumi tu wakiwa wazima na nyoka wakubwa hadi urefu wa mita 7.6.

Remove ads

Mwainisho

  • Nusuoda: Serpentes
    • Oda ya chini: Caenophidia
      • Familia ya juu: Acrochordoidea
        • Familia: Acrichordidae
      • Familia ya juu: Colubroidea
      • Familia ya juu: Elapoidea
        • Familia: Atractaspididae (Afrika na Asia) - matandu, vizambarau, walanyoka
        • Familia: Elapidae (Afrika, Asia, Australia na Marekani) - fira, futa, hongo
        • Familia: Lamprophiidae (Afrika)
        • Familia: Prosymnidae (Afrika)
        • Familia: Psammophiidae (Afrika, Asia na Ulaya)
        • Familia: Pseudaspididae (Afrika)
        • Familia: Pseudoxyrhophiidae (Afrika na Marekani)
      • Familia ya juu: Homalopsoidea
        • Familia: Homalopsidae (Asia na Australia)
      • Familia ya juu: Pareatoidea
        • Familia: Pareatidae (Asia)
      • Familia ya juu: Viperoidea
      • Familia ya juu: Xenodermatoidea
        • Familia: Xenodermatidae (Asia)
    • Oda ya chini: Henophidia
      • Familia ya juu: Booidea
        • Familia: Aniliidae (Amerika ya Kusini)
        • Familia: Anomochilidae (Asia)
        • Familia: Boidae (Afrika, Asia, Marekani na Ulaya) - sundakuwili
        • Familia: Pythonidae (Afrika, Asia na Australia) - chatu
        • Familia: Bolyeriidae (Afrika)
        • Familia: Cylindrophiidae (Asia)
        • Familia: Loxocemidae (Amerika ya Kati)
        • Familia: Tropidophiidae (Marekani)
        • Familia: Uropeltidae (Asia)
        • Familia: Xenopeltidae (Asia)
    • Oda ya chini: Scolecophidia
Remove ads

Marejeo

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

Ukweli wa haraka
Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyoka kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads