From Wikipedia, the free encyclopedia
Otilia wa Alsasya (pia Odilia wa Alsace; 662 hivi - Mont Sainte-Odile, 720 hivi) alikuwa mwanamke wa ukoo maarufu wa Alsace (leo nchini Ufaransa).
Inasemekana alikataliwa na baba yake kwa sababu ya jinsia yake na ya upofu wake, hivyo alilelewa na wakulima.[1]
Miujiza mbalimbali ilitokea katika maisha yake baada ya kupata ubatizo na kuwezeshwa kuona.
Alianzisha monasteri mbili na kuwa abesi wake.
Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu. Mwaka 1807 Papa Pius VII alithibitisha heshima hiyo.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 13 Desemba[2].
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Every time you click a link to Wikipedia, Wiktionary or Wikiquote in your browser's search results, it will show the modern Wikiwand interface.
Wikiwand extension is a five stars, simple, with minimum permission required to keep your browsing private, safe and transparent.