24 (msimu wa 8)
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Msimu wa nane, pia hujulikana kama Siku ya nane, ya televisheni ya Marekani ya kipindi cha 24 ilianza kutayarishwa mnamo 27 Mei 2009, na itaonyeshwa kwa mara ya kwanza tarehe 17 Januari 2010, kufuatia muundo wa kipindi hiki tangu msimu wa nne. [1]
Remove ads
Hadithi
Hadithi kuu itahusisha Jack Bauer akipambana na vitisho vya mauaji vilivyofanywa wakati wa mkutano wa amani kati ya Rais Allison Taylor wa Marekani na Rais Omar Hassan wa Jamhuri Kiislamu ya Kamistan(nchi hii si ya ukweli bali ya mwandishi wa kipindi hiki). [2] [3]
Msimu wa kipindi hiki utahamishiwa mji wa New York na huko afisi ya CTU itafunguliwa upya, [4] lakini Kutokana na vikwazo vya bajeti,hakutakuwa na kurekodi matukio yoyote katika mji huu wa New York . [5]
Matukio yataanza na kumalizika saa kumi za jioni. [6][7]
Imefunuliwa kwamba Gregory Itzin atarudia jukumu lake la kumwigiza Rais mstaafu Charles Logan wakati fulani katika msimu huu. [8]
Remove ads
Watayarishi
Msimu wa nane utayarishwa na televisheni ya 20th Century Fox na Imagine. Mahojiano ya hivi karibuni, Kiefer Sutherland alithibitisha kwamba msimu wa nane utafanyika punde tu baada ya matukio ya kufunga ule msimu wa saba. Kulingana na Keifer Sutherland, msimu huu unaweza kuwa wa mwisho kama waandishi hawatakuja na mawazo mazuri ya msimu wa tisa kama mashabiki wanataka mwigizo zaidi. Sutherland alisema "kuna mengi sana unaeza kumfanyia Jack (Bauer) kabla ya kupoteza ukweli wa mambo. Nadhani filamu itakuwa njia nzuri ya kumaliza hadithi hii. "
Waandalizi na waandishi Howard Gordon, Evan Katz, David Fury, Regine Coto, Brannon Braga, Brad Turner, Alex Gansa, Brian Grazer, Chip Johannessen na Patrick Harbinson washasainishwa kwa ajili ya msimu wa nane.
Pia miongoni mwa waandalizi wa kuu ni mwigizaji mkuu Kiefer Sutherland. [9]
Remove ads
Waigizaji
Waigizaji wakuu
- Kiefer Sutherland kama Jack Bauer [10]
- Mary Lynn Rajskub kama Chloe O'Brian [10]
- Anil Kapoor kama Rais Omar Hassan [10]
- Annie Wersching kama Renee Walker [10]
- Mykelti Williamson kama mkuu wa New York CTU Brian Hastings [10] [11]
- Katee Sackhoff kama Dana Walsh [10]
- Chris Diamantopoulos kama mkuu wa wafanyikazi wa White House Rob Weiss [10]
- John Boyd kama Arlo Glass [10]
- Freddie Prinze, Jr kama Cole Ortiz [10]
- Cherry Jones kama Rais Allison Taylor [10]
Waigizi wasaidizi
- Daudi Anders kama Josef Bazhaev [12]
- Nazneen Contractor kama Kayla Hassan [13] [14]
- Elisha Cuthbert kama Kim Bauer [15]
- Bob Gunton kama Katibu Mkuu wa Jimbo Ethan Kanin [16]
- Gregory Itzin kama Charles Logan [17]
- Domenick Lombardozzi kama John Mazoni [18]
- Benito Martinez kama Victor Aruz [19]
- Callum Keith Rennie kama Vladimir Laitanan [20]
- Stephen Root kama Ben Prady [21]
- Paulo Wesley kama Stephen [22]
- Jennifer Westfeldt kama Meredith Reed [23]
- Johnny Wu kama Phillip Lu [18]
Video fupi
Video fupi ya kwanza iliekwa kwenye tovuti,fox.com, tarehe 28 Oktoba 2009. Video fupi iliitwa "Survive" yani kuishi tena. Mjukuu wa Jack anaonekana kuwa mkubwa kidogo kuliko alivyokuwa katika mwisho wa msimu wa saba. Pia video fupi hii inaonyesha Jack akiwa na hamu ya kurudi California na familia yake, lakini kabla ya kufanya hivyo hana budi "kuvumilia siku moja zaidi". Video hii pia inamwonyesha Chloe akifanya kazi CTU na huku akizungumza na Jack kwa simu. [24]
Remove ads
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads