Adamu mpya
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Adamu mpya, Adamu wa pili au Adamu wa mwisho (1Kor 15:45) ni kati ya majina ya Yesu katika Agano Jipya.[1][2][3]


Humo mara mbili Mtume Paulo anafananisha Yesu na Adamu.
Katika 1Kor 15:22 anasema, "kama vile katika Adamu wote wanakufa, vivyo hivyo katika Kristo wote watafanywa hai" na katika mstari wa 45 unamuita Yesu "Adamu wa mwisho".
Halafu katika Rom 5:12–21 anasema, "kama vile kwa kosa la mtu mmoja wengi wamefanywa wakosefu, vivyo hivyo kwa utiifu wa mmoja wengi watafanywa waadilifu" (Rom 5:19).
Remove ads
Katika teolojia
Kutokana na Yesu kuitwa Adamu mpya, Bikira Maria alifananishwa na Eva kuanzia karne ya 2 (Irenei), kwa jinsi alivyoshirikiana naye kama Eva mpya.
Katika Kurani
Quran pia inafananisha Yesu na Adamu kwa jinsi walioumbwa[4].
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads