Ait Benhaddou

From Wikipedia, the free encyclopedia

Ait Benhaddou
Remove ads

Aït Benhaddou (kwa Kiberber: ⴰⵢⵜ ⴱⴻⵏⵃⴰⴷⴷⵓ; kwa Kiarabu: آيت بن حدّو) ni ksar au mji-ngome katika Moroko ya kusini. Zamani ilipitiwa na njia ya misafara baina ya maeneo ya jangwa la Sahara na mji wa Marrakesh.

Thumb
Ait Benhaddou
Thumb
Nyumba kubwa ya Ait Benhaddou

Ait Benhaddou iko takriban kilomita 100 upande wa kusini-magharibi wa Marrakesh kando ya mto wenye maji kwenye miezi ya mvua.

Wenyeji ni Waberber waliojenga makazi yao kwa namna ya ngome. Nyumba za familia huwa na ghorofa tatu au zaidi, zimejengwa kwa kutumia udongo ulioshindiliwa na kuwa tayari ya kuishi mle, kuhifadhi bidhaa na kujitetea dhidi ya mashambulio. Nyumba kubwa zilijengwa na wafanyabiashara walioshiriki katika misafara.

Katika karne ya 20 wenyeji walianza kutoka kwenye nyumba za kale na kujenga kijiji kipya kando ya makazi ya zamani. Lakini watalii wengi wanakuja kuangalia mfano huu wa ubunifu wa kihistoria uliopokewa katika orodha ya UNESCO ya urithi wa dunia tangu mwaka 1987.[1]

Remove ads

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads