Amman

From Wikipedia, the free encyclopedia

Amman
Remove ads

Amman (kwa Kiarabu: عمان ʿammān) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Yordani wenye wakazi milioni nne katika rundiko la mji.

Thumb
Msikiti wa Mfalme Abdullah
Ukweli wa haraka Habari za msingi, Mahali ...
Remove ads

Jiografia

Mji uko takriban km 40 kutoka ncha ya kaskazini ya Bahari ya Chumvi kati ya vilima vya Yordani ya kaskazini-magharibi.

Hali ya hewa ni afadhali kushinda mahali pengi pa Yordani kwa sababu ya kimo cha mji, hivyo joto halizidi mno.

Historia

Amman ni mji wenye historia ndefu iliyojulikana kwa jina la Rabat Amon wakati wa Biblia.

Ilistawi vizuri hadi nyakati za Dola la Roma ilipopambwa na majengo makubwa na mazuri yanayoonekana hadi leo.

Lakini umuhimu wake ulipungua siku za Wamuawiya na wakati wa kuundwa kwa Yordani palikuwa kijiji tu. Mfalme Abdullah bin al-Husayn alianzisha hapa mji mkuu wake. Hadi vita kuu ya pili ya dunia Amman haikuzidi wakazi 30,000.

Lakini mji ulikua haraka baada ya kuundwa kwa Israeli kwa sababu wakimbizi wengi kutoka sehemu za Palestina zilizokuwa Israeli walikimbilia Amman.

Kipindi cha pili cha kukua kilitokea tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe ya Lebanoni miaka ya 1975-1990. Sehemu kubwa ya benki na biashara kutoka Beirut ilihamia Amman iliyoendelea kuwa kitovu kipya cha biashara na uchumi upande wa mashariki wa Mediteranea.

Remove ads

Picha za Amman

Viungo vya nje

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Amman kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads