Andrea Corsini

From Wikipedia, the free encyclopedia

Andrea Corsini
Remove ads

Andrea Corsini, O.Carm. (30 Novemba 13026 Januari 1373/1374) alikuwa Mkarmeli wa Italia aliyehudumia kama askofu wa Fiesole tangu mwaka 1349 hadi kifo chake.

Thumb
Mt. Andrea Corsini akisali - Guido Reni (1630-1635).

Akiwa kijana aliishi vibaya hadi karipio la mama yake lilipomfanya aamue kuingia utawani aliposhika maisha magumu na kutafakari sana Biblia.

Baada ya kushika nafasi mbalimbali shirikani, akirekebisha konventi zilizoharibiwa na tauni, alikubali kwa shida uaskofu akaongoza kwa busara jimbo lake akiongeza juhudi zake za kiroho na matendo ya huruma kwa maskini na kupatanisha maadui.

Tangu kale aliheshimiwa na waumini na hatimaye Papa Eugenio IV alimtangaza mwenye heri tarehe 21 Aprili 1440 na Papa Urban VIII alimtangaza mtakatifu tarehe 22 Aprili 1629.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads