Andrea Tuong

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Andrea Tuong (1812-1862) alikuwa mkulima ambaye alifungwa pamoja na tabibu Dominiko Nguyen, na wakulima wenzake Dominiko Nhi, Dominiko Mao na Vinsenti Tuong kwa ajili ya imani ya Kikristo.

Baada ya kuteswa kwa muda mrefu gerezani, walikatwa kichwa chini ya kaisari Tu Duc[1].

Ni kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 16 Juni[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads