Dominiko Nguyen
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dominiko Nguyen (1802-1862) alikuwa tabibu ambaye alifungwa pamoja na wakulima Dominiko Nhi, Dominiko Mao, Vinsenti Tuong na Andrea Tuong kwa ajili ya imani ya Kikristo.
Baada ya kuteswa kwa muda mrefu gerezani, walikatwa kichwa chini ya kaisari Tu Duc[1].
Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 16 Juni[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads