Ansar al-Sunna Msumbiji

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Ansar al-Sunna Msumbiji (kwa Kiar. أنصار السنة, 'Wasaidizi wa mapokeo'), wanaojulikana pia kama al-Shabaab, Ahlu al-Sunna, Wasunna Waswahili, [1] na Ahlu Sunna wal Jammah, ni kundi la wanamgambo wa Kiislamu wanaopatikana katika Mkoa wa Cabo Delgado kaskazini mwa Msumbiji. [2] Kundi hilo limeshambulia vikosi vya usalama na raia katika jaribio la kuanzisha serikali ya Kiislamu katika eneo hilo. [3] [4] [5]

Remove ads

Jina

Katika mapokeo ya Uislamu jina "ansar" linarejelea kundi la Waarabu waliomsaidia mtume Muhammad alipofika Madina. Sunna inataja mapokeo ya Muhammad na namna jinsi alivyotenda.

Jina la Ansar al-Sunna ni sawa na jina la kundi la waasi nchini Iraki ambalo lilipambana na jeshi la Marekani mnamo 2003 hadi 2007. Wenyeji wanawaita "al-Shabaab" lakini hao ni tofauti na Al-Shabaab wa Somalia. [6] Dola la Kiislamu (Daish) limewahi kudai eti ni tawi lao lakini dai hilo halikuweza kuthibitishwa. Hata hivyo, kuna dalili kwamba Ansar al-Sunna walipokea usaidizi fulani kutoka Daish.

Remove ads

Historia

Inasemekana kundi hilo lilianzishwa huko Cabo Delgado na wafuasi wa mhubiri Mkenya Aboud Rogo Mohammed waliohamia Msumbiji baada ya kifo cha mwalimu wao mnamo 2012. [7] Kundi lilivuta vijana wasio na ajira na walalahoi katika eneo hili kama vile wavuvi, wafanyabiashara ndogondogo, na wachimbaji wa madini ambao walihisi kupuuzwa na serikali ya Msumbiji. Kundi lilizidi kuwa na vurugu mnamo 2017, likianza kushambulia vituo vya polisi na ofisi za serikali. [7] Mashambulio hayo yalizidi katika miaka iliyofuata, pamoja na kulenga masoko, shule na vijiji ambako walinyimwa usaidizi.

Thumb
Maeneo yaliyodhibitiwa na Ansar al-Sunna mnamo Septemba 2020 (kijivu)

Tangu mwaka 2020 Ansar al-Sunna walifaulu kuvamia pia miji midogo na kuitetea kwa muda dhidi ya jeshi la Msumbiji na makundi ya mamluki kutoka Urusi na Afrika Kusini walioajiriwa na makampuni ya gesi na madini katika mkoa huo. Kwa muda walidhibiti maeneo ya pwani pamoja na mji wa Mocimboa da Praia.

Mwezi wa Machi 2021 walifaulu kuteka pia mji wa Palma na kuishika wiki mbili dhidi ya jeshi la Msumbiji lilofaulu kuwaondoa kwa msaada kutoka Afrika Kusini. Tangu Julai 2021 kikosi cha majeshi ya nchi za SADC kilianza kufika na wanajeshi wa Rwanda walifaulu kuondoa wanamgambo kutoka sehemu kubwa ya eneo walilowahi kudhibiti.

Remove ads

Mandharinyuma

Sababu kuu ya kufaulu kwa uasi huo ni hali tata ya uchumi kwenye mkoa wa Cabo Delgado. Tofauti na Msumbiji kwa jumla, wenyeji wengi ni Waislamu na mkoa huo haujaona uwekezaji mkubwa kutoka serikali kuu. Maafisa wa serikali walionekana kama wanatafuta rushwa. Makambi ya makampuni ya kigeni yanayotafuta gesi na madini yalianzishwa lakini hayakuleta bado faida kwa wenyeji. Kuna taarifa kuwa polisi na wanajeshi wa serikali waliwatenda wenyeji kwa ukali pamoja na kuua vijana hovyo baada ya kushambuliwa na wanamgambo wa Ansar al-Sunna, hali iliyofanya wengine kujiunga nao[8].

Mapato yao hutokana na biashara ya magendo na mitandao ya kidini. [9]

Wanamgambo wa Ansar al-Sunna wanaripotiwa kuwa wengi wao ni Wamsumbiji kutoka wilaya za Mocímboa da Praia, Palma na Macomia, lakini ni pamoja na raia wa kigeni kutoka Tanzania na Somalia. Wanamgambo hao wameripotiwa kuzungumza Kireno, lugha rasmi ya Msumbiji, Kimwani, lugha ya kienyeji, na Kiswahili. [10]

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads