Al-Shabaab
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Kuhusu Al-Shabaab nchini Msumbiji tazama Ansar al-Sunna Msumbiji

Al-Shabaab (kwa Kiarabu: الشباب, "Vijana"; kirefu: حركة الشباب المجاهدين, Ḥarakat ash-Shabāb al-Mujāhidīn; kifupisho: HSM; kwa Kisomali: Xarakada Mujaahidiinta Alshabaab; maana yake "Tapo la Vijana wa Jihad") ni kundi la Waislamu wenye itikadi kali lililoanzishwa nchini Somalia mwaka 2006 kutokana na Islamic Courts Union (ICU)[1].
Mwaka 2012 lilijiunga na Al-Qaeda.[2][3][4][5].
Wanamgambo wa Al-Shabaab walikadiriwa kuwa 7,000 - 9,000 mwaka 2014, wakiwemo wageni wengi, hasa kutoka Yemen, Sudan, Kenya, Tanzania, Afghanistan, Saudi Arabia, Malaysia, Pakistan na Bangladesh[6].
Mwaka 2015 waliacha miji yote muhimu na kuendelea kutawala maneno machache ya vijijini tu.[7]
Hata hivyo wanaendelea kupigana na wanaotazamwa nao kama maadui wa Uislamu hasa nchini Somalia, Kenya na Yemen. Kundi linaloitwa Al-Shabaab nchini Msumbiji lilianzishwa kwa njia tofauti, si tawi la Al-Shabaab wa Somalia.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads