Antoni Daniel

From Wikipedia, the free encyclopedia

Antoni Daniel
Remove ads

Antoni Daniel, S.J. (Dieppe, Ufaransa 25 Mei 1601 karibu na Teanaostaye, Kanada, 4 Julai 1648) alikuwa padri wa Wajesuiti mmisionari kwa Wahuroni wa Amerika Kaskazini tangu mwaka 1632[1].

Thumb
Wajesuiti wafiadini wa Amerika Kaskazini.

Aliuawa kwa mishale na Wairoki, kabila lingine la Waindio, akisimama mlangoni mwa kanisa alipomaliza kuadhimisha Misa na akiwa na lengo la kulinda waumini wapya. Hatimaye alichomwa moto.

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930.

Sikukuu ya kundi lake la wafiadini huadhimishwa tarehe 19 Oktoba, lakini ya kwake mwenyewe huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads