Koikoi
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Koikoi ni ndege wakubwa wa jenasi Ardea katika familia ya Ardeidae wenye miguu mirefu na domo refu na nyembamba. Hupinda shingo yao wakiruka angani. Ndege hawa wana rangi nyeupe, kijivu na nyeusi. Spishi zenye rangi ya kahawiachekundu huitwa pondagundi pia. Spishi mbili nyeupe kabisa zinaitwa msuka na yangeyange. Zamani msuka ilikuwa imeainishwa ndani ya jenasi Egretta na yangeyange ndani ya jenasi Bubulcus. Kuna spishi nyingine za yangeyange ndani ya jenasi mbalimbali. Koikoi hupenda kula samaki lakini hula wanyama wadogo pia, kama vyura, mijusi, nyoka na panya. Hujenga matago yao kwa matawi juu ya miti. Jike huyataga mayai 2-6.
Remove ads
Spishi za Afrika
- Ardea alba, Msuka (Great White Egret)
- Ardea a. alba, Msuka wa Ulaya (Eurasian Great White Egret)
- Ardea a. melanorhynchos, Msuka wa Afrika (African Great White Egret)
- Ardea brachyrhyncha, Koikoi domo-njano (Yellow-billed Egret)
- Ardea cinerea, Koikoi Kijivu (Grey Heron)
- Ardea c. cinerea, Koikoi Kijivu (Grey Heron)
- Ardea c. firasa, Koikoi Kijivu wa Visiwa (Indian Ocean Grey Heron)
- Ardea goliath, Pondagundi Mkubwa au Koikoi Jitu (Goliath Heron)
- Ardea humbloti, Koikoi wa Madagaska (Humblot's Heron)
- Ardea ibis, Yangeyange au Yange Fuatang'ombe (Western Cattle Egret)
- Ardea melanocephala, Koikoi Majoka (Black-headed Heron)
- Ardea purpurea, Pondagundi (Purple Heron)
- Ardea p. bournei, Pondagundi wa Kaboverde (Cape Verde Purple Heron)
- Ardea p. madagascariensis, Pondagundi wa Madagaska (Madagascar Purple Heron)
- Ardea p. purpurea, Pondagundi (Purple Heron)
Remove ads
Spishi za mabara mengine
- Ardea cocoi (Cocoi Heron)
- Ardea coromanda (Eastern Cattle Egret)
- Ardea herodias (Great Blue Heron)
- Ardea insignis (White-bellied Heron)
- Ardea intermedia (Intermediate Egret)
- Ardea pacifica (White-necked or Pacific Heron)
- Ardea picata (Pied Heron)
- Ardea plumifera (Plumed Egret)
- Ardea sumatrana (Great-billed Heron)
Spishi za kabla ya historia
- Ardea bennuides (Bennu Heron)
- Ardea formosa
- Ardea howardae
- Ardea polkensis (Mwanzo wa Pliocene ya Bone Valley, MMA)
- Ardea similis
- Ardea sp. (Kati ya Miocene ya Observation Quarry, MMA)
- Ardea sp. (Mwisho wa Miocene ya Love Bone Bed , MMA)
- Ardea sp. (Mwanzo wa Pleistocene ya Macasphalt Shell Pit, MMA)
Picha
- Msuka
- Yange fuatang'ombe
- Koikoi kijivu
- Pondagundi mkubwa
- Koikoi wa Madagaska
- Koikoi domo-njano
- Koikoi majoka
- Pondagundi
- Cocoi heron
- Great blue heron
- White-bellied heron
- White-necked heron
- Pied heron
- Plumed egret
- Great-billed heron
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads