Basilika la Mt. Paulo

From Wikipedia, the free encyclopedia

Basilika la Mt. Paulo
Remove ads

Basilika la Kipapa la Mt. Paulo Nje ya Kuta ni mojawapo kati ya mabasilika ya zamani na muhimu zaidi ya Roma[1] pamoja na yale ya Mt. Yohane huko Laterano, Mt. Petro huko Vatikano na Mt. Maria huko Eskwilino.

Thumb
Upande wa mbele wa Basilika-
Thumb
Mlango mtakatifu.
Thumb
Mosaiki ya mwaka 1220 ikimuonyesha Kristo kati ya mitume Petro na Paulo, Mtume Andrea na Mwinjili Luka.
Thumb
Undani wa kanisa.
Thumb
Ramani ya basilika
Thumb
Sibori ya Arnolfo di Cambio.
Thumb
Mt. Paulo Nje ya Kuta.
Thumb
Nguzo za nje.

Basilika liko katika eneo la Italia[2], lakini Ukulu Mtakatifu unalimiliki kabisa[3]kama ilivyo kwa maeneo ya balozi za nchi ya kigeni.[4]

Remove ads

Historia

Basilika lilianzishwa na kaisari Konstantino Mkuu juu ya mahali (cella memoriae) alipozikwa Mtume Paulo baada ya kukatwa kichwa nje ya ngome ya jiji la Roma.[5][6][7][8][9][10]

Baada ya mabadiliko mengi, lilijengwa upya katika karne ya 19 kwa sababu lilikuwa limeteketezwa na moto. Vipimo vyake ni mita 131.66 kwa 65 kwa 29.70, hivyo ni kanisa la pili kwa ukubwa mjini Roma.

Kumbukumbu ya kutabarukiwa kwake inafanyika kila mwaka tarehe 18 Novemba[11] pamoja na ya kutabarukiwa Basilika la Mt. Petro ili kudokeza udugu wa Mitume hao wawili na umoja wa Kanisa lote [12].

Tangu mwaka 1980 Basilika hilo liko katika orodha ya UNESCO ya Urithi wa Dunia.

Remove ads

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads