Mtume Andrea
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mtume Andrea alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmoja kati ya wawili wa kwanza kati ya Mitume wa Yesu.


Anaheshimiwa na Wakristo wote kama mtakatifu, hasa tarehe 30 Novemba iliyo sikukuu yake[1].
Ni msimamizi wa Uskoti, Russia, Ugiriki, Romania, Malta, Prussia, wa jimbo la Konstantinopoli na wa mabaharia, wavuvi, na waimbaji.
Remove ads
Asili na jina
Inakadiriwa alizaliwa mwaka 6 K.K. huko Bethsaida akauawa 60 hivi huko Patras (Ugiriki).
Jina lake asili la Kiyahudi halijulikani. Kwa Kigiriki aliitwa Ανδρέας (Andreas, maana yake Mwanamume, Rijali). Anaitwa pia Protocletos yaani Wa kwanza kuitwa (na Yesu Kristo).
Agano Jipya linasema Andrea alikuwa ndugu wa Mtume Petro, mwana wa Yona au Yohana (Math 16:17; Yoh 1:42).
Wito wake

Wote wawili walihamia Kafarnaumu ili kufanya kazi ya uvuvi, na ndipo walipoitwa na Yesu kuwa "wavuvi wa watu" (ἁλιείς ἀνθρώπων, halieis anthropon).
Injili ya Yohane inaarifu kuwa Andrea aliwahi kuwa mwanafunzi wa Yohane Mbatizaji, mpaka nabii huyo alipomuelekeza amfuate Yesu Kristo, "Mwanakondoo wa Mungu" atakayekamilisha kazi yake mwenyewe (Yoh 1:35-40). Andrea akiwa wa kwanza kumtambua Yesu kuwa Masiya, alimtambulisha kwa ndugu yake hukohuko kwenye mto Yordani (Yoh 1:41).
Ni baada ya hapo kwamba waliitwa kuacha yote wamfuate Yesu (Mk 1:17-18; Math 4:19-20; Lk 5:11).
Remove ads
Baada ya ufufuko wa Yesu
Katika Injili Andrea anatajwa mara kadhaa kuwa karibu sana na Yesu (Mk 13:3; Yoh 6:8, 12:22), lakini katika Matendo ya Mitume anatajwa mara moja tu, katika orodha ya Mitume (1:13).
Mwanahistoria Eusebius wa Kaisarea anataja Asia Ndogo, Skizia, pwani ya Bahari Nyeusi na mto Volga hadi Kiev kuwa mahali pa utume wake baada ya ufufuko wa Yesu.
Mapokeo mengine yanadai alifanya utume sehemu za Akaya (Ugiriki) akasulubiwa huko Patras juu ya msalaba wenye umbo la X uliopewa jina lake[2].
Apokrifa za Andrea
Kati ya vitabu vilivyokataliwa na Kanisa (Decretum Gelasianum ya Papa Gelasio I) kuna Injili ya Andrea na Matendo ya Andrea vilivyoandikwa karne ya 3.
Picha
- Ndugu Limbourg, Kifodini cha Mt. Andrea, toka Les Très Riches Heures du duc de Berry, Chantilly, Musée Condé
- José de Ribera, Kifodini cha Mt. Andrea, 1628, Budapest, Szépmüvészeti Múzeum.
- Kifodini cha Mt. Andrea, karne XII, Presencio.
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads