Bata Mzinga
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Mabata mzinga au mapiru (kwa Kiingereza anaitwa turkey) ni ndege wakubwa wa jenasi Meleagris, jenasi pekee ya nusufamilia Meleagridinae katika familia Phasianidae. Ndege hawa ni wakubwa kabisa kati ya Phasianidae.
Makala hii inahitaji vyanzo zaidi ili kuwezesha kuonyesha uthibitisho. |

Wanafanana kidogo na bata, wana manyoya ya kahawia,kichwa kisicho na manyoya na shingo yenye ngozi ya makunyazi isiyo na manyoya. Kichwa chao hakina manyoya na kina rangi nyekundu, pinki au ya kijivu. Manyoya yana rangi nyeusi imetayo yenye madoa.
Hula makokwa, mbegu, beri, mizizi na wadudu, pengine amfibia na watambaachi.
Jike hutaga mayai 10-14 huku wengine kufikia hadi idadi ya mayai 20, katika shimo la kina kifupi. Makinda hutoka tago katika masaa 12-24.
Remove ads
Spishi
- Meleagris gallopavo, Bata Mzinga Mwitu (Wild Turkey)
- Meleagris g. gallopavo f. domesticus, Bata Mzinga Kaya ( Domesticated Turkey)
- Meleagris ocellata, Bata Mzinga Mkia-madoa (Ocellated Turkey)
Spishi za kabla ya historia
Picha
- Bata mzinga mwitu
- Bata mzinga mkia-madoa
![]() |
Makala hii kuhusu ndege fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Bata Mzinga kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads