Beatriz wa Silva
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Beatriz wa Silva, O.I.C. (jina kamili kwa Kireno: Beatriz de Menezes da Silva; Campo Maior, Ureno[1] 1424 hivi – Toledo Hispania, 9 Agosti 1492) alikuwa mwanamke wa ukoo maarufu wa Ureno, lakini alijiunga na monasteri na hatimaye akawa mwanzilishi wa masista wamonaki wa Shirika la Bikira Maria Kukingiwa Dhambi ya Asili.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira.
Remove ads
Maisha

Beatriz alizaliwa Campo Maior; kati ya ndugu zake 10, mmojawapo ni mwenye heri Amadeo wa Ureno, aliyerekebisha shirika la Ndugu Wadogo.
Mwaka 1447 Beatriz alihamia katika ikulu ya Kastilia ili kumsindikiza rafiki yake Isabela aliyeolewa na mfalme wa huko.[3]
Lakini uzuri wa Beatriz ulimtia kijicho, hata akamfunga katika chumba kidogo.
Humo Beatriz alitokewa na Bikira Maria na kuelekezwa aanzishe shirika jipya kwa heshima yake.
Beatriz alipofaulu kutoroka alikimbilia monasteri ya Wadominiko wanawake (Utawa wa pili) huko Toledo, akaishi huko miaka 37 bila kujiunga nao kisheria.[3][4]
Mwaka 1484 Beatriz na wenzake kadhaa walitamalaki monasteri nyingine ya Toledo aliyopewa na malkia ili itumike kuheshimu Kukingiwa Dhambi ya Asili Bikira Maria.
Mwaka 1489, kwa ruhusa ya Papa Innocent VIII, walipokea sheria za Wasitoo,[3] wakiahidi kuadhimisha kila siku Breviari ya Bikira Maria Mkingiwa Dhambi ya Asili, wakiwa chini ya askofu mkuu wa Jimbo kuu la Toledo.

Remove ads
Baada ya kifo
Mwaka 1501 Papa Alexander VI aliunganisha jumuia hiyo na Wabenedikto lakini chini ya Kanuni ya Mt. Klara.
Mwaka 1511 Papa Julius II aliwapa kanuni mpya ya kwao, halafu kardinali Fransisko Quiñones aliwaandikia katiba maalumu.
Kuanzia mwaka 1507 shirika lilienea Ureno, Hispania, Italia, Ufaransa na Brazil.
Beatriz wa Silva alitangazwa mwenye heri tarehe 28 Julai 1926 na Papa Pius XI, halafu mtakatifu na Papa Paulo VI tarehe 3 Oktoba 1976.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads