Benedikto Yosefu Labre

From Wikipedia, the free encyclopedia

Benedikto Yosefu Labre
Remove ads

Benedikto Yosefu Labre (kwa Kifaransa Benoît-Joseph Labré; Amettes, Boulogne-sur-Mer, Ufaransa, 25 Machi 1748 - Roma, Italia, 16 Aprili 1783) alikuwa Mkristo ambaye tangu ujanani alitamani sana maisha ya toba kali.

Thumb
Mtakatifu Benedikto Yosefu alivyochorwa na Antonio Cavallucci mwaka 1795.
Thumb
Mtakatifu Benedikto Yosefu Labre.
Thumb
Kanisa la Santa Maria ai Monti alimozikwa.

Kwa ajili hiyo aliiishi miaka mingi bila makao maalumu, akihiji kwa tabu nyingi makanisa mbalimbali akiwa amevaa nguo zilizochakaa na akila alichopewa tu, akitoa mfano bora wa ibada, hasa kwa kuabudu ekaristi.

Hatimaye alihamia Roma alipoishi katika sala na ufukara mkubwa sana [1].

Alitangazwa na Papa Pius IX kuwa mwenye heri tarehe 20 Mei 1859, halafu Papa Leo XIII akamtangaza mtakatifu tarehe 8 Desemba 1881.

Sikukuu yake ni tarehe 16 Aprili[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads