Bethsaida
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bethsaida (kutoka Kiebrania/Kiaramu בית צידה beth-tsaida, yaani "Nyumba ya uwindaji" au "ya uvuvi", kutoka mzizi צדה auצוד)[1] ni mahali panapotajwa na Agano Jipya.
Palikuwa upande wa mashariki wa mto Yordani, labda jirani na mahali ambapo mto huo unaingia katika Ziwa Galilaya. [2]
Bethsaida ndio mji asili wa mitume wa Yesu wafuatao: Petro, Andrea nduguye na Filipo (Yoh 1:44).
Bethsaida inatajwa na Mk 8:22-26 kama mji (κώμη) ambapo Yesu alimponya kwa awamu mbili mwanamume kipofu.
Ingawa katika Injili hakuna habari za miujiza mingine iliyofanyika huko, Yesu aliutishia mji huo laana ya milele kwa kutopokea ujumbe wake wa toba.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads