Birisi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Birisi
Remove ads

Birisi ni nyoka wasio na sumu wa familia Typhlopidae. Kwa lugha nyingine huitwa “nyoka vipofu” mara nyingi, kwa sababu hawana macho au macho yamepunguka mpaka madoa meusi yanayoweza kulinganua nuru na giza tu. Spishi moja, birisi tingatinga, imeainishwa katika familia Xenotyphlopidae.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Nyoka hawa ni wafupi na wembamba, sm 95 kwa kipeo lakini sm 30-50 kwa kawaida. Spishi fupi sana ni birisi-Asia mdogo (sm 5-15) na huyu ni nyoka mfupi kabisa duniani. Rangi yao ni nyeusi, kijivu, kahawia au pinki pengine pamoja na madoa au mabaka.

Birisi huchimba ardhini, huingia vishimo au hujificha chini ya mawe au magogo, mara nyingi magogo yaliyooza. Kwa hivyo hawahitaji macho. Hula mchwa hasa.

Nyoka hawa hawana sumu na kwa kisa chochote mdomo wao ni mdogo sana; kwa hivyo hawawezi kung'ata mtu na wanaweza kukamatwa bila shida.

Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Picha

Marejeo

  • Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.

Viungo vya nje

Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Birisi kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads