Bulawayo
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Bulawayo ni mji mkubwa wa pili wa Zimbabwe wenye wakazi 665,940 (sensa ya 2022[1]). Iko kusini-magharibi ya nchi hiyo, katikati ya Matabeleland. Wakazi walio wengi ni Wandebele.



Jina la mji linatokana na neno la Kindebele "Kwabulawayo" yaani "machinjoni".
Remove ads
Historia
Mji wa leo ulijengwa juu ya mabaki ya boma la mfalme Lobengula. Lobengula aliwahi kujenga boma lake la kwanza 1871 takriban kilomita 15 kusini ya mji. Mwaka 1881 alihamia penye mji wa sasa.
Mwaka 1893 ufalme wa Lobengula ulishambuliwa na jeshi la Cecil Rhodes na mfalme aliamua kuchoma boma lake alipoona alishindwa kuzuia maadui. Waingereza walianzisha mji wao juu ya mabaki ya makazi ya awali. 1897 ilipewa cheo cha manisipaa na kuungwa na reli.
Bulawayo ilikuwa mji ambako upinzani dhidi ya ukoloni ulianza na baadaye kitovu cha upinzani dhidi ya serikali ya Robert Mugabe.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads