Kamerun

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kamerun
Remove ads

Kamerun, rasmi inajulikana kama Jamhuri ya Kamerun (Kifaransa: République du Cameroun), ni nchi iliyoko Afrika ya Kati. Kamerun Ina idadi ya watu takriban milioni 28, na inashika nafasi ya 54 kwa kuwa na idadi kubwa ya watu duniani. Inapakana na Nijeria upande wa magharibi, Chad upande wa kaskazini-mashariki, Jamhuri ya Afrika ya Kati upande wa mashariki, Jamhuri ya Kongo na Gabon upande wa kusini, na Guinea ya Ikweta upande wa kusini-magharibi. Nchi hii pia ina pwani kwenye Bahari ya Atlantiki upande wa magharibi. Inajumla ya eneo la takriban kilomita za mraba 475,442, na hivyo kuwa mojawapo ya nchi kubwa zaidi barani Afrika. Mji mkuu na jiji kubwa zaidi ni Yaounde, ambalo ni kituo cha kisiasa na utawala cha nchi hiyo.

Ukweli wa haraka Jamhuri ya Kameruni République du Cameroun (Kifaransa)Republic of Cameroon (Kiingereza), Mji mkuu ...
Remove ads

Jiografia

Thumb
Mpare kwa mlima Kameruni
Makala kuu: Jiografia ya Kamerun
Thumb
Mlima Kamerun kutoka Tiko, Mkoa wa Kusini-Magharibi

Maeneo kiutawala

Makala kuu: Mikoa ya Kamerun na Wilaya za Kamerun

Kameruni imegawiwa katika mikoa (regions) 10 na wilaya (départements) 58.

Mikoa ni:


Ona pia: Orodha ya miji ya Kameruni

Historia

Historia ya awali

Katika karne za BK Wabantu wenye ujuzi wa kilimo na uhunzi walianza uenezi wao kutoka huko kwenda kutawala maeneo mengi ya Afrika ya Kati, Kusini mwa Afrika na Afrika Mashariki.

Wakati wa ukoloni

Kameruni ilikuwa koloni la Ujerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baada ya Ujerumani kushindwa vita, nchi ikagawiwa kati ya Uingereza na Ufaransa chini ya mamlaka ya Shirikisho la Mataifa kama eneo la kudhaminiwa.

Tangu uhuru hadi leo

Mwaka wa 1960, Wafaransa waliacha Kameruni ikawa nchi huru. Wananchi wa Kameruni ya Kiingereza walipiga kura kuamua kama walitaka kuwa sehemu ya Nigeria au ya Kameruni. Kaskazini wengi walipendelea kukaa Nigeria, hivyo maeneo hayo sasa ni sehemu ya Nigeria. Wananchi wengi wa kusini waliamua wajiunge na Kameruni[4]. Kwa kusudi la kuheshimu tofauti za kiutamaduni kulikuwa na katiba mpya kwenye mwaka 1961 Shirikisho la Jamhuri ya Kameruni.

Tangu 1972 muundo wa nchi ulibadilishwa kuacha mfumo wa shirikisho na kuwa jamhuri ya muungano inayokazia zaidi matumizi ya lugha ya Kifaransa ingawa Kiingereza bado ni moja ya lugha rasmi. Jina la nchi pia likabadilishwa kuwa Jamhuri ya Muungano ya Kameruni mwaka wa 1972. Hapo sehemu ya Wakamerun wanaotumia lugha ya Kiingereza walijisikia kuwa wananyimwa haki zao.[5] Baadaye, mwaka wa 1984 jina likabadilishwa tena kuwa Jamhuri ya Kameruni (kwa Kifaransa République du Cameroun).

Tangu mwaka 2016 upinzani uliongezeka kati ya watu wa magharibi wanaotumia Kiingereza. Harakati hiyo ilijibiwa na serikali na polisi kwa ukali na hii umeleta kuanzishwa kwa wanamgambo wenye silaha wanaoshambulia polisi na jeshi la serikali kuu. Tangu mwaka 2017 wapinzani wamedai uhuru wa sehemu yenye lugha ya Kiingereza wakitangaza wameunda nchi mpya ya "Ambazonia". Serikali iliundwa inayokaa Nigeria; lakini kuna vikundi tofauti ambavyo wanapigana kati yao[6]. Nchi hii haitambuliwi kimataifa. Mwaka 2021 kulikuwa na majadiliano kuhusu amani kati kundi linalojiita serikali ya Ambazonia na serikali ya Kameruni[7], lakini makundi mengine yaliendelea na mapigano ya silaha[8].

Remove ads

Siasa

Thumb
Rais wa Kameruni Paul Biya (kulia)
Makala kuu: Siasa za Kamerun

Uchumi

Thumb
Majani chai inayotoka Kameruni
Makala kuu: Uchumi wa Cameroon

Watu

Thumb
Yaoundé, mji mkuu wa Kameruni (2003)
Thumb
Picha, kaskazini mwa Kameruni
Thumb
Ikulu ya sultani wa Bamun kwa Foumban, Mkoa wa Magharibi
Makala kuu: Watu wa Kamerun na Orodha ya lugha za Kamerun

Wakazi walikuwa 22,534,532 mwaka 2013, ambao wamegawanyika sawasawa kati ya wanaoishi mijini na wale wa vijijini.

Lugha rasmi ni Kifaransa pamoja na Kiingereza. Hata hivyo wakazi wanaongea pia lugha za makabila yao mengi.

Upande wa dini, 70% ni Wakristo (40% Wakatoliki na 30% Waprotestanti), 18% ni Waislamu, 3% ni wafuasi wa dini asilia za Kiafrika. 6% hawana dini yoyote.

Remove ads

Utamaduni

Thumb
Nyumba ya Njem
Thumb
Mwanamke wa Maka akienda shamba
Thumb
Familia ya Tikar, Kaskazini magharibi
Makala kuu: Utamaduni wa Kamerun, Muziki wa Kamerun, Mapishi ya Kamerun, na Waandishi wa Kamerun

Elimu

Makala kuu: Elimu Kamerun

Tazama pia

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads