Kirukanjia Meno-meupe

From Wikipedia, the free encyclopedia

Kirukanjia Meno-meupe
Remove ads

Virukanjia meno-meupe au virukanjia-zabadi ni wanyama wadogo wa nusufamilia Crocidurinae katika familia Soricidae wanaofanana na vipanya, lakini virukanjia si wagugunaji (oda Rodentia). Spishi hizi zinatokea Afrika, Asia na Ulaya ya kusini. Nusufamilia hii ina spishi ndogo kuliko virukanjia wote (kirukanjia wa Etruski aliye na 3.5 sm) na ile kubwa kuliko wote (Kirukanjia-kaya wa Asia aliye na sm 15). Spishi za Crocidurinae zina meno meupe, kinyume na zile za Soricinae ambazo zina meno mekundu, na zina harufu ya zabadi pia. Zina miiba mgongoni inayoonekana zikiogopa au zikikasirika. Rangi yao ni nyeusi, kijivu au kahawia. Hula wadudu, konokono na nyungunyungu hasa lakini mbegu na makokwa pia.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...

Kama ni lazima watoto wahamishwe, mama na watoto huunda mnyororo au msafara, kila mnyama akishikilia yule mbele yake. Mwenendo huu umeonwa pia miongoni mwa spishi kadhaa za jenasi Sorex. Virukanjia meno-meupe wana akili kama ile ya mbwa. Wameonwa wakishirikiana katika kundi.

Remove ads

Spishi za Afrika

Remove ads

Spishi za Asia na Ulaya

Remove ads

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads