D

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

D ni herufi ya 4 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Delta ya alfabeti ya Kigiriki.

Maelezo zaidi Alfabeti ya Kilatini, (Kwa matumizi ya Kiswahili) ...

Maana za D

Historia ya D

Maelezo zaidi Hieroglifu ya Misri mlango, Kisemiti asilia Mlango (wa hema) ...

Asili ya herufi D ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na alama ya "dalet" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya mlango wakitumia alama tu kwa sauti ya "d" na kuiita kwa neno lao kwa mlango "dalet". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "Delta" bila kujali maana asilia ya "mlango" ilikuwa sauti tu ya "d".

Waitalia wa kale kama Waetruski wakapokea herufi kwa umbo lisilokuwa na kona kali. Waroma wakaichukua lakini waligeuza mwelekeo wake kuwa D jinsi ilivyo hadi sasa.

Remove ads
Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads