R

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

R ni herufi ya 18 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Rho ya Kigiriki.

Maelezo zaidi Alfabeti ya Kilatini, (Kwa matumizi ya Kiswahili) ...

Maana za alama R

Historia ya herufi R

Maelezo zaidi Kisemiti asilia kichwa (resh), Kifinisia resh (R) ...

Asili ya herufi R ni miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na alama ya "resh" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya kichwa wakitumia alama tu kwa sauti ya "r" na kuiita kwa neno lao kwa kichwa yaani "resh". Wagiriki walichukua alama hiyo wakaigeuza na kuiita "rho" bila kujali maana asilia ya "kichwa" ilikuwa sauti tu ya "r".

Waitalia wa kale kama Waetruski wakapokea herufi kwa umbo lililofanana zaidi na Kifinisia. Waroma wakaichukua lakini waligeuza mwelekeo wake kutazama upandde wa kulia wakaongeza mkono mdogo kuwa mguu wa pili kwa kutoifautisha na P.

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads