Dominiko Dinh Dat

From Wikipedia, the free encyclopedia

Remove ads

Dominiko Dinh Dat (1803-1839) alikuwa askari Mkristo wa Vietnam. Akilazimishwa kwa mateso makali, alikanyaga msalaba wa Yesu, lakini alitubu haraka akamuandikia kaisari Minh Mang kwamba anataka kuhukumiwa tena kwa imani yake, na hatimaye alinyongwa[1].

Ni mmojawapo kati ya wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe ni tarehe 18 Julai[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads