Dominiko Pham Thong
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dominiko Pham Thong (1780-1859) ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Pamoja na mwanae Luka Thin Viet Pham (1819-1859) na Yosefu Pham Thong Ta (1800-1859) aliteswa vikali na hatimaye kufia dini huko Nam Dinh, Vietnam Kaskazini kwa kuwa walikataa kukanyaga msalaba [1].
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, ila ya kwake ni tarehe 13 Januari[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads