Dominiko Savio
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dominiko Savio (Kiitalia: Domenico Savio; Riva presso Chieri, 2 Aprili 1842 – Castelnuovo Don Bosco, 9 Machi 1857[1][2]) alikuwa mvulana wa Italia aliyelelewa na Yohane Bosco kufuata upole na furaha na kwa njia hiyo alifikia mapema ukamilifu wa Kikristo [3].

Akiwa anasomea upadri aliugua na hatimaye akafariki dunia katika umri wa miaka 14 tu.[4]
Mlezi wake aliandika kitabu juu yake (Maisha ya Dominiko Savio) ambacho kilichangia sana kumfanya ajulikane na hatimaye atangazwe na Papa Pius XII kwanza mwenye heri tarehe 5 Machi 1950, halafu mtakatifu[5] tarehe 12 Juni 1954.[6]
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads