Dominiko Toai
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Dominiko Toai (1811/1812 - 1862) alikuwa mvuvi na baba wa familia. Ingawa alifungwa muda mrefu na kuteswa kwa namna mbalimbalichini ya kaisari Tu Duc, pamoja na Dominiko Huyen walihimiza kwa ushujaa wafungwa wenzao wadumu katika imani, wakikamilisha ushuhuda wao kwa kuchomwa moto [1].
Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (1625–1886).
Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.
Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.
Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 5 Juni[2].
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Marejeo ya lugha nyingine
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads