Domomwiko

Jenasi ya ndege wakubwa wa maji wenye domo la umbo la mwiko From Wikipedia, the free encyclopedia

Domomwiko
Remove ads

Domomwiko ni ndege wa nusufamilia Plataleinae katika familia ya Threskiornithidae ambao wana miguu mirefu na domo lenye umbo wa mwiko. Rangi yao ni nyeupe isipokuwa Roseate Spoonbill ambaye ana rangi ya pinki. Hulipeleka domo lao huku na huku katika maji machache na wakisikia kiumbe mdogo kama samaki mdogo, mdudu au gegereka, hulifunga upesi ili kukamata windo. Hujenga tago lao juu ya miti au matete, mara nyingi pamoja na kwarara, yangeyange na koikoi. Jike huyataga mayai 2-5.

Maelezo zaidi Uainishaji wa kisayansi, Ngazi za chini ...
Remove ads

Spishi za Afrika

Spishi za mabara mengine

Picha

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads