Dr. Dre
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Andre Romelle Young (alizaliwa tar. 18 Februari 1965) ni mtayarishaji wa rekodi, rapa, na mmiliki wa studio ya rekodi za muziki kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Dr. Dre. Dre ni mwanzilishi na mmiliki wa sasa Aftermath Entertainment na mmiliki mshiriki-msanii wa zamani wa studio ya Death Row Records, na pia kutayarisha albamu kadhaa kwa ajili yake na wasanii wengine kadhaa wa rekodi hiyo kama vile Snoop Dogg na Eminem.
Akiwa kama mtayarishaji, amejipatia sifa sana kwa kuukuza muziki wa West Coast G-funk, staili ya muziki wa rap unaotengenezwa na synthesizer-yenye ya taratibu, na mdundo wa nguvu.
Dr. Dre alianza shughuli za muiki akiwa kama mmoja kati ya wanamchama wa kundi la muziki la World Class Wreckin' Cru na kisha baadaye akaanzisha kundi lenye athira kubwa ya gangsta rap la N.W.A, ambayo ilivuma sana kwa mashairi yake mazito yenye kutaja maisha ya kiharifu na mtaani kwa ujumla.[1] Mnamo mwaka wa 1992, alitoa albamu kama msanii wa kujitegemea. Na albamu ilikwenda kwa jina la The Chronic, ilitolewa ikiwa chini ya Death Row Records, na kumpelekea kuwa mmoja katia ya wasanii waliouza rekodi bora za muziki wa Marekani kwa mwaka wa 1993[2] na kushinda Tuzo ya Grammy kwa ajili ya single ya "Let Me Ride".
Mnamo mwaka wa 1996, aliondoka Death Row na kwenda kuanzisha studio yake mwenyewe ya Aftermath Entertainment, na kutoa albamu ya mchanganyiko ya Dr. Dre Presents the Aftermath, kunako 1996, na ksiha baadaye akatoa albamu yake nyingine iliyokwendwa kwa jina la 2001, kunako 1999, ambayo ili mfanya ashinde Tuzo ya Grammy akiwa kama mtayarisha bora.
Kunako miaka ya 2000, aliekeza shughuli zake za utayarishaji wa muziki kwa wasanii wengine, wakati muda huo akawa anashiriki katika kutia sauti kwenye baadhi ya nyimbo za wasanii wengine.
Rolling Stone wamemwita ni mmoja kati ya wasanii waliolipwa pesa nyingi sana kwa mwaka wa 2001[3] na 2004.[4] Dr. Dre also had acting roles in the 2001 films The Wash and Training Day.[5]
Remove ads
Wasifu
Maisha ya awali
Alizaliwa akiwa kama mtoto wa kwanza wa Verna na Theodore Young, Dr. Dre alizaliwa na jina la André Romelle Young mnamo tar. 18 Februari 1965, wakati mama yake akiwa na umri wa miaka 16. Ameolewa na baba yake, Theodore Young, baada ya kuzaliwa kwake. Jina lake la kati, "Romelle," linatoka katika jina la Theodore Young, ambalo ni jina la kundi la kuimba muziki wa R&B wa lidhaa, The Romells. Mnamo mwaka wa 1968 mama yake akatarikiwa na Theodore Young na kisha baadaye akaja kuoelewa na Curtis Crayon. Kwa pamoja wakaja kuzaa tena mitoto mitatu, wawili wa kiume Jerome na Tyree (wote wamefariki) na binti mmoja aliyeitwa Shameka.
Mnamo mwaka wa 1976 Young akapata kujiunga na shule ya Vanguard Junior High School, lakini kwa kufuatia vurugu, fujo na uhuni uliojaa katika shule ya Vanguard, akahamishwa katika kitongoji kilichosalama kabisa katika shule ya Roosevelt Junior High School.[6] Baadaye Verna akajakuolewa na Warren Griffin, ambaye alikutana naye katika eneo la kazi yake mpya huko Long Beach,[7] ambaye yeye ndiye aliongeza madada wengine watu na mkaka mmoja katika familia. Huyo ndugu wa kiume, Warren Griffin III, ambaye baadaye alikuja kuwa na rapa na kujiita Warren G.[8]
Young alielekeza zake tena katika shule ya Centennial High School ya mjini Compton wakati wa ujana wake mnamo mwaka wa 1979, lakini alihamisha katika shule ya Fremont High School kwa kufuatia viwango vidogo. Young akathubutu kujiandikisha katika kampuni moja iitwayo Northrop Aviation Company kwa mpango wa kujiendeleza kivitendo, lakini viwango vidogo vya shuleni vimefanya awe hafai. Baada ya hapo, akaamua kulenga maisha yake ya kijamii katika masuala ya burudani kwa ajili ya maisha yake ya shule.[9] Young akapata mtoto wa kiume, Curtis, aliyezaliwa tar. 15 Desemba 1981, na Lisa Johnson. Curtis Young alilelewa na mama yake na hajaonana na baba yake hadi Curtis alipokuja kuwa rapa akiwa na umri wa miaka 20 hapo baadaye, akiwa na jina la kisanii la Hood Surgeon.[10]
Remove ads
Muziki
Albamu
Albamu za studio
- The Chronic (1992)
- 2001 (1999)
- Compton (2015)
Albamu za filamu
- The Wash (2001)
Albamu za ushirikiano
akishirikiana na World Class Wreckin' Cru
- World Class (1985)
- Rapped in Romance (1986)
akishirikiana na N.W.A.
- N.W.A. and the Posse (1987)
- Straight Outta Compton (1988)
- 100 Miles and Runnin' (1990)
- Niggaz4Life (1991)
Tuzo na mapendekezo
Tuzo za Grammy
Dr. Dre ameshinda Tuzo za Grammy mara sita. Tatu kati ya hizo ni kwa kazi yake ya utayarishaji.[11][12][13]
MTV Video Music Awards
Remove ads
Filamu
Remove ads
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads