Emanueli Le Van Phung

From Wikipedia, the free encyclopedia

Emanueli Le Van Phung
Remove ads

Emanueli Le Van Phung (1796-1859) alikuwa baba wa familia na katekista wa Vietnam ambaye alifungwa gerezani miezi saba pamoja na padri Petro Qui Cong Doan kwa sababu ya imani yake kwa Yesu. Akiwa huko aliendelee kuhimiza wanae tisa na ndugu wengine kuwapenda watesi wake hadi walipokatwa kichwa wote wawili kwa amri ya kaisari Tu Duc[1].

Thumb
Sanamu yake na ya mfiadini mwenzake.

Ni mmojawapo kati ya Wakristo wafiadini wa Vietnam waliouawa kwa ajili ya imani yao huko Vietnam katika karne ya 17, 18 na 19 (16251886).

Wanatajwa pia kama Watakatifu Andrea Dũng-Lạc na wenzake 116.

Kwa nyakati tofauti, Papa Leo XIII, Papa Pius X na Papa Pius XII waliwatangaza kuwa wenye heri, halafu Papa Yohane Paulo II aliwaunganisha katika kuwafanya watakatifu wafiadini tarehe 19 Juni 1988.

Sikukuu yao huadhimishwa kwa pamoja kila tarehe 24 Novemba, ila ya kwake mwenyewe tarehe 31 Julai[2].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo ya Kiswahili

Marejeo ya lugha nyingine

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads