Erkonvaldi

From Wikipedia, the free encyclopedia

Erkonvaldi
Remove ads

Erkonvaldi (kwa Kiingereza: Earconwald, Ercenwald, Erkenwald; Lindsey[1], karne ya 7 - monasteri ya Barking, 30 Aprili 693) alikuwa askofu wa London, Uingereza, kuanzia mwaka 675[2] akawa mwanzilishi wa monasteri mbili za Kibenedikto[3][1][4]. Ile ya kike iliongozwa na dada yake, Etelburga wa Barking, ila ya kiume iliongozwa naye mwenyewe[5].

Thumb
Mt. Erkonvaldi na Mt. Wiliamu katika dirisha la kioo cha rangi.

Tangu kale anaheshimiwa kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki na Waanglikana tarehe ya kifo chake[6].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads