Esuperansi wa Cingoli

From Wikipedia, the free encyclopedia

Esuperansi wa Cingoli
Remove ads

Esuperansi wa Cingoli (alizaliwa Afrika Kaskazini - alifariki Cingoli, Marche, Italia) alikuwa askofu wa mji huo mwishoni mwa karne ya 5[1].

Thumb
Sanamu ya Mt. Esuperansi huko Cingoli (karne ya 12).

Tangu zamani anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu[2].

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe 24 Januari[3].

Maisha

Mtoto wa familia ya Wamani na Waario, alikubaliwa na baba yake kupata ubatizo katika Kanisa Katoliki akiwa na umri wa miaka 12.

Baada ya kukomaa, aliishi kimonaki na kuinjilisha maeneo ya Afrika Kaskazini.

Alipotaka kuhamia Italia na kufika Roma alikamatwa, lakini Papa alifaulu kumtoa akamfanya askofu wa Cingoli. Huko alifanya kazi miaka 15 hadi kifo chake akiwa na sifa ya kufanya miujiza[4].

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Viungo vya nje

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads