Exit 13
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Exit 13 ni albamu ya kumi na mbili (ya 13 kwa ujumla) na albamu ya mwisho ya LL Cool J kujihusisha na studio ya rekodi ya Def Jam Recordings, uhusisho ambao ulidumu kwa takriban miaka kumi na miwili. Awali albamu ilipewa jina la Todd Smith Pt. 2: Back to Cool. Albamu ilitolewa mnamo tar. 9 Septemba 2008.
Remove ads
Matayarisho
Albamu ni ya kwanza kwa albamu za LL Cool J tangu G.O.A.T. kuwa na nembp ya parental advisory kwa mashairi makali. Kwenye mahojiano ya redio yaliyofanywa na DJ Z kule mjini Chicago, LL alisema kwamba maneno yasiyo ya adabu si mabaya sana. Badala ya kutoimba maneno haya mabaya, toleo lililohaririwa linatumia mashairi mengine badala ya yale yasiyo ya adabu.[1] LL na DJ Kayslay wameungana ili kuweza kutoa albamu yao ya kwanza ya mixtape ukiwa kama utangulizi wa jina la Exit 13 liopewa jina la The Return of the G.O.A.T..
Wachangiaji wengie wa katika albamu hii ni pamoja na 50 Cent, Sheek Louch, Fat Joe, Ryan Leslie, Wyclef Jean, The-Dream, Lil Mo, Grandmaster Caz, Funkmaster Flex, Richie Sambora na Darlisa Blackshere.
Remove ads
Single
Toleo lisilo rasmi la single ya mtaani, "Rockin' with the G.O.A.T.," ilianza kutolewa kwa mara ya kwanza mnamo tar. 20 Juni 2008.
Toleo rasmi la single ya kwanza, "Baby" akimshirikisha The-Dream ilitolewa mnamo tar. 1 Julai 2008 kupitia Maduka ya Muziki ya iTunes. Mnamo tar. 19 Agosti 2008, iTunes wametoa remixi ya ya rock akimshirikisha Richie Sambora, ikiwa na mahadhi ya rock na mistari ya kasi kidogo.
Toleo rasmi la single ya pili, "Feel My Heart Beat" akimshirikisha 50 Cent ilitolewa mnamo tar. 26 Agosti 2008. Lakini kwa bahati mbaya wimbo haukiingia katika chati za Billboard Hot 100. Toleo rasmi la wimbo huo ulivuja kwenye mtandao wa intaneti mnamo tar. 27 Novemba 2008.
Remove ads
Orodha ya nyimbo
Chati
Marejeo
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads