Visiwa vya Falkland
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Visiwa vya Falkland (kwa Kiingereza: Falkland Islands; kwa Kihispania Islas Malvinas) ni funguvisiwa katika bahari ya Atlantiki ya kusini takriban km 450 mbele ya pwani ya Argentina.


Falkland ni eneo la ng'ambo la Uingereza linalodaiwa na Argentina kama sehemu yake. Hivyo mwaka 1982 jeshi la Argentina ilivamia visiwa vikuu. Uingereza ilijibu kivita ikapeleka wanajeshi huko na baada ya vita vifupi vya wiki 6 Argentina ilishindwa; takriban wanajeshi 1,000 waliuawa.
Remove ads
Jiografia
Funguvisiwa lina takriban visiwa 200. Viwili ambavyo ni vikubwa ni Falkland Magharibi na Falkland Mashariki na kila kimoja huwa na eneo la takriban km² 6,000. Mwinuko mkubwa ni mlima Usborne (Kihispania: Cerro Alberdi) wenye kimo cha mita 708 juu ya uwiano wa bahari.
Hali ya hewa ni baridi na kuna mvua nyingi. Halijoto ya wastani ni 5 °C pekee. Kwa sababu hiyo mimea ni hasa nyasi; kutokana na baridi miti haizidi kimo cha mita 1.
Remove ads
Watu
Idadi ya wakazi imepita 3,000 na wote hao ni Waingereza wanaosema Kiingereza. Wanajipatia riziki zao kwa uvuvi na ufugaji wa kondoo.
Upande wa dini, 66% ni Wakristo, hasa Waanglikana, lakini pia Wakatoliki na wengineo. 32% hawana dini yoyote.
Mji pekee ambao ni pia makao makuu ya utawala ni Port Stanley kwenye kisiwa cha mashariki wenye wakazi 2,100. Pamoja na wakazi kuna wanajeshi Waingereza 1,500.
Barabara ya lami ya pekee kisiwani ni ile inayounganisha Stanley na kituo cha kijeshi kwa umbali wa kilomita 50.
Remove ads
Tanbihi
Marejeo
Viungo vya Nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads