Filipo Howard

From Wikipedia, the free encyclopedia

Filipo Howard
Remove ads

Filipo Howard (28 Juni 155719 Oktoba 1595) alikuwa mtu wa ukoo maarufu nchini Uingereza na binamu wa Malkia Elizabeti I.

Thumb
Mt. Filipo Howard alivyochorwa.

Baada ya kuishi kwa anasa katika ikulu, alipata uongofu wa kimaadili aliposikiliza hoja za mapadri Wakatoliki (1581) na hatimaye aliacha madhehebu ya Anglikana ajiunge na Kanisa Katoliki, ingawa kwa siri, kutokana na dhuluma ya serikali.

Hatimaye alikamatwa na kufungwa hadi kifo chake miaka 10 baadaye[1]. Gerezani alishangaza watu kwa jinsi alivyoishi katika sala na matendo ya toba hadi alipokwisha kwa kuteswa na kwa kukosa mahitaji [2].

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 15 Desemba 1929, halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 alimtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39[3].

Sikukuu yake ni tarehe ya kifodini chake[4].

Remove ads

Tazama pia

Tanbihi

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads