Fort Portal

From Wikipedia, the free encyclopedia

Fort Portal
Remove ads

Fort Portal au Kabarole ni mji wa kitalii uliopo Mkoa wa Magharibi, Uganda. Ndio mji mkuu wa Wilaya ya Kabarole. Ndipo panapopatikana ufalme wa Toro.[1][2]

Ukweli wa haraka Nchi, Mkoa ...
Thumb
Mji wa Fort Portal
Remove ads

Mahali

Mji wa Fort Portal upo umbali wa takribani kilomita 296 magharibi mwa Kampala. Kampala mji mkuu wa Uganda na pia jiji kubwa zaidi la nchi hiyo.Majiranukta ya Fort Portal ni 0°39'16.0" kas, 30°16'28.0"Mas (Latitudo:0.654444; Longitudo:30.274444).Mji wa Fort Portal upo katika mwinuko wa mita 1523 kutoka kwenye usawa wa bahari.[3]

Idadi ya watu

Kwa mujibu wa sensa ya kitaifa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa Fort Portal ilikuwa 41,000. Mwaka 2010, shirika la takwimu la Uganda lilikadiria kuwa wakazi wa mji huo ni takribani 46,300. Mwaka 2011, shirika hilo lilikadiria idadi ya wakazi kufika 47,100.[4] Mwezi Agosti, mwaka 2014, Sensa ya kitaifa ya makazi ilidhihirisha idadi ya wakazi kufikia 54,275.[5]

Tazama pia

Marejeo

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads