Fransiska wa Roma
From Wikipedia, the free encyclopedia
Remove ads
Fransiska wa Roma (kwa Kiitalia Francesca Romana; 1384 – 9 Machi 1440) alikuwa mtawa kutoka Roma, Italia.


Ametambuliwa na Kanisa Katoliki chini ya Papa Paulo V kuwa mtakatifu kuanzia tarehe 29 Mei 1608.
Maisha
Fransiska alizaliwa katika mji wa Roma, Italia, mwaka 1384.
Aliolewa mapema mwaka 1396, akazaa watoto watatu. Katika miaka 40 ya ndoa yake alijitokeza kama mke na mama bora. Alijulikana sana kwa moyo wake wa ibada, unyenyekevu, upole, uvumilivu na kujitoa kwake mhanga kuwasaidia maskini. Aliishi nyakati ngumu, hivyo aliwapatia mali yake, na kuuguza wagonjwa.
Mwaka 1425 alianzisha Shirika la Waoblati waliofuata Kanuni ya Mt. Benedikto na baada ya kifo cha mumewe akajiunga nao. Alifariki dunia mwaka 1440.
Remove ads
Tazama pia
Tanbihi
Marejeo ya Kiswahili
Viungo vya nje
Wikiwand - on
Seamless Wikipedia browsing. On steroids.
Remove ads