Funguvisiwa la Lamu

From Wikipedia, the free encyclopedia

Funguvisiwa la Lamumap
Remove ads

Funguvisiwa la Lamu ni kundi la visiwa katika Bahari Hindi mbele ya pwani ya Kenya kaskazini ambavyo ni sehemu ya Kaunti ya Lamu, Kenya.

Thumb
Ramani ya funguvisiwa la Lamu: Lamu, Manda, Pate.

Visiwa vikubwa ni Pate, Manda na Lamu. Visiwa vidogo ni pamoja na Kiwayu na Manda Toto.

Mji mkubwa zaidi ni Lamu kwenye Kisiwa cha Lamu. Mji huu uko katika orodha ya Urithi wa dunia ya UNESCO.

Funguvisiwa la Lamu lina sehemu mbalimbali zenye mabaki muhimu ya kiakiolojia kutoka vyanzo vya utamaduni wa Waswahili kama vile Takwa na mji wa Manda halafu Shanga, Pate.

Kuna taarifa ya kwamba jahazi za kundi la meli la Zheng He zilizama karibu na Lamu mnamo mwaka 1415.[1] Mabaharia wa jahazi hizi walibaki kwenye visiwa na kuoa wanawake wa huko. Uchunguzi wa DNA wa wenyeji umethibitisha kuwepo kwa damu ya Kichina.[2] [3][4]

Remove ads

Picha

Tazama pia

Marejeo

Kujisomea

Loading related searches...

Wikiwand - on

Seamless Wikipedia browsing. On steroids.

Remove ads